TUKIO LIJALO • UPCOMING
Kongamano la Ufalme wa Mungu
06 - 09 OCTOBER 2026 • Kanisa la Shekina, Kunduchi Mtongani
KUHUSU SISI

Kristokrasia ni nini?

Kristokrasia (Christocracy) maana yake ni Utawala wa Kristo. Sisi ni chombo huru cha waumini, wachungaji na viongozi wanaofundisha, wanaoishi na wanaosimamia Ufalme wa Mungu katika familia, kanisa na jamii.

KUHUSU CHRISTOCRACY

Utawala wa Kristo

Christocracy maana yake ni Utawala wa Kristo — Kristo akitawala moyoni, nyumbani, kanisani na katika jamii. Ufalme wa Mungu si mahali pa mbali tu; ni utawala na mamlaka ya Mungu yanayotenda kazi hapa duniani kupitia watu wake.

Yohana Mbatizaji aliandaa njia ya Ufalme, Yesu akahubiri Ufalme, na sisi tumetumwa kuhubiri Ufalme ule ule: “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mathayo 10:7)

✦Kristokrasia ni chombo huru — si kanisa wala dhehebu, na hakimilikiwi na kanisa lolote. Tunatumika pamoja na makanisa yote yanayotaka kujengwa katika Ufalme.
Nembo ya CPCT
Tunashirikiana na CPCT
Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania — tazama madhehebu yake yote →
DIRA • VISION
Kizazi kinachojua mamlaka yake katika Kristo na kinachotawala kwa haki, hekima na uwajibikaji.
DHAMIRA • MISSION
Kufundisha Injili ya Ufalme, kuandaa wachungaji na viongozi, na kujenga kanisa la nyumbani lenye afya — “kwa ajili ya kujengwa kwa Ufalme wa Mungu.”
TUNAAMINI • WE BELIEVE
  • ✦Kusudi la Mungu tangu mwanzo ni utawala. “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu… wakatawale.” (Mwanzo 1:26-28)
  • ✦Nchi amewapa wanadamu. “Mbingu ni mbingu za BWANA, bali nchi amewapa wanadamu.” (Zaburi 115:16)
  • ✦Yesu alikuja kurejesha Ufalme — alivyokuja, alivyokufa na alivyoondoka vyote vinashuhudia kusudi hilo. (Warumi 5:14-19)
  • ✦Tumefanywa ufalme na makuhani kwa Mungu, nasi tutamiliki juu ya nchi. (Ufunuo 1:5-6; 5:9-10)
  • ✦Tunaombea na kutenda: “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.” (Mathayo 6:10)
Somo: Ufahamu wa Ufalme
Kingdom Mindset — Mch. Daniel Mulesi
↗
TUNACHOFANYA

Njia nne tunazojenga
Ufalme pamoja

01
Mafunzo ya Ufalme
Madarasa na semina za kina kuhusu Ufalme wa Mungu, mamlaka ya muumini na uongozi wa kiroho.
02
Kuandaa Wachungaji
Mafunzo maalumu kwa wachungaji, wazee wa kanisa na viongozi — kwa nidhamu na uwajibikaji.
03
Kanisa la Nyumbani
Kujenga familia zinazoabudu, zinazoombeana na zinazolea kizazi kijacho katika Neno.
04
Makongamano
Mikutano ya kila mwaka inayounganisha makanisa na kuwajenga waumini kwa pamoja.

Ungana nasi katika kujenga Ufalme